Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 08 -- Sixth Commandment: Do Not Murder
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule? -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

08 - Amri Ya Sita: Usiue



KUTOKA 20:13
“Usiue”


08.1 - La kushangaza, hata hivyo ni kweli

Mwanadamu wa kwanza aliyezaliwa na mwanamke na kupendwa na baba yake akawa ni mwuaji wa ndugu yake. Biblia laonyesha wazi hilo tendo la hila la kuvunja sheria na uasi yenye mizizi ya chini ndani ya moyo wa binadamu. Watu wote hubeba ndani yao tabia ya kurithiwa ya mwuaji. Tangu Adamu, mwanadamu ameishi katika hali ya kutengwa na Mungu akiwa mtu wa kujisifu kabisa (egoisti) na kuongozwa na tamaa na tumaini zake mwenyewe. Anafikiri isivyotambulika vizuri hata kwake mwenyewe kwamba, yeye ndiye wa katikati na wa kuangaliwa kama mfano wa kufaa kwa wengine. Anapotokea mwingine na kuonekana kuwa mwenye nguvu zaidi, akili zaidi, mcha Mungu zaidi au mzuri zaidi, anamwonea wivu na kumchukia. Kila mtu binafsi hutamani kuwa nusu mungu akishangazwa, hata kuabudiwa na wengine. Lakini kiburi na kujidai kuwa mwenye haki yeye tu, hii ni tabia ya kuharibu.

Yesu amtaja shetani kuwa ni “mwuaji tangu mwanzo”, maana alimwondoa mwanadamu kutoka kwa ushirikiano wake wa awali pamoja na Mungu. Tangu hapo basi, kifo umetawala binadamu, “ maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Ila Mungu ametutayarishia njia ya kuweza kurudi kwake kwa uwezo wa upendo na haki zake. Yeyote atakaye kuchukua faida ya nafasi hiyo ya kuokoka, akifanywa upya nafsini mwake na kumpokea Mungu kuwa lengo la maisha yake, basi atapokea uzima wa milele hata leo. Hayo yatampatia shabaha na maana maishani mwake.

Mwanadamu anayo kisa na sababu nyingi za kuua. Yesu aliweka wazi kwamba, uuaji ndiyo la kwanza katika mawazo mabovu yote yatokayo ndani ya moyo wa binadamu (Mathayo 15:9). Lakini katika utakatifu wake Mungu akakemea makusudi mabaya ya mtu na kumkataza kutimiza shabaha zake alipoamuru, “Usiue”! Kwa sababu hiyo, namna zozote za kuua, hata kujiua mwenyewe, ni kinyume cha mapenzi ya Mungu na kuhesabiwa kwamba si jambo dogo, ila ni uasi dhidi ya Mungu mwenyewe. Zaidi ya hapo, ikiwa mtu anamtendea mwenzake vibaya, bila kujali kama anaona njaa au bila kumwonya akiingia hatari fulani, basi huyu naye anahesabiwa katika ujumla wa wauaji. Ikiwa yeyote anamjeruhi mtu, au kutia sumu katika chakula chake, au kumtia moyo mtu mwingine aue, basi ataketishwa kwenye msululu wa wauaji wote wenye kungojea hukumu ya milele. Hata kama mtu atamwumiza mwingine na kwa njia hiyo kufupisha maisha yake, yeye naye ni mwuaji kufuatana na Biblia (Warumi 13:1-18). Mungu atuhesabia kuwa tunawajibika kwa ajili ya wenzetu, hivyo hatuwezi kujiudhuru na kusema alivyotamka Kaini, “Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”


08.2 - Malipo na Kisasi

Hukumu ya kifo ndani ya Agano la Kale ilitolewa kama tisho la kuogofya, pia na kuwa timizo la haki dhidi ya kila mwuaji na mwuaji wa siri (Kutoka 21:12,14,18). Zamani zile karibu watu wote waliishi ndani ya makabila yaliyolinda usalama kama bima ya uhai. Hofu la kuhusishwa katika uadui wa kikabila unaomwaga damu ulipata kuwa namna ya ulinzi kwa mtu binafsi. Ile sheria inayotamka, “jicho kwa jicho na jino kwa jino” ilipanga aina ya malipo kwa kiasi cha ukubwa wa dhuru uliotendeka. Lakini malipo yangezidishwa mara nyingi ikiwa mkuu wa kabila aliuawa. Lameki alidai watu 77 wauawe ikiwa yeye atauawa (Mwanzo 4:23-24). Makabila kadhaa bado wanatumia hayo, kama kuna uuaji wa mmoja wa viongozi wao.

Katika utamaduni wa kishemu uuaji ni tendo la kuvunja sheria isiyoweza kusamehewa wala haiwezi kuridhishwa ila kwa kumwaga damu ya huyu mtu. Kusamehe ingekuwa si haki. Watu huchukua faida kutokana na kujisikia kuwa na hatia ya wengine. Chuki juu ya adui itatunzwa toka kizazi hadi kizazi, hata ikiwa taifa nzima itahusishwa. Mawazo kama hayo yamepata kuwa geni kwa Wakristo, wakiwa wakiishi mashariki au magharibi. Sisi tunao utamaduni iliyo tofauti tangu Kristo alipomwaga damu yake, ili afute hatia ya kila mwuaji.

Mwuaji huendelea kujisikia vibaya kwa vile analemazwa na hatia yake. Roho za wale aliyewaua zitamwinda mawazoni wake au katika ndoto. Usiku fulani wakati wa vita kuu ya pili askari mwenye kuwapiga mmoja mmoja kwa bunduki aliona vichwa vya wale aliyewaua vinavingirishwa kuelekea kwake na macho yao matupu yakimvizia. - Kama mwuaji anarudi nyumbani kwake kwenye kijiji chake cha kiislamu, hata kama ni baada ya kizazi kizima, lazima atazamie kuuawa na mwana wa yule aliyemwua. Uuaji hauna faida. Hata hivyo, haitoshi kuwatia hofu au kuwatisha watu kwa ajili ya kuwazuia wasiue. Mawazo yote maovu lazima yaondolewe mioyoni mwa watu na badala yake wapewe mawazo masafi mapya. Yesu alifahamu makusudi ya moyo wa binadamu, na katika hali hiyo kwa ndani alimhukumu kila mmoja kustahili kufa aliposema, „Aliye mwema ni mmoja, ambaye ni Mungu“ (Mathayo 19:17; Marko 10:18; Luka 18:19). Lakini wakati uo huo yeye mwenyewe alibeba hatia zetu kama wauaji na kututia Roho yake tamu mioyoni mwetu, inayoweza kufanya kuwa mpya mioyo yetu na kuondoa mawazo ya kuua. Yesu hutupatia moyo mpya na roho iliyo ya kweli, na kutufanya tuwe waumini wawezao kutii maagizo yake, hata tuweze kupenda adui zetu.


08.3 - Mtazamo wa Kikristo kuhusu Uuaji na Upatanisho

Katika hotuba yake ya mlimani Yesu alitufundisha kwamba, kuua mwili sio pekee tendo la kuvunja amri, bali masingizio pia inahesabiwa kuwa kuua roho wa mtu. Matokeo yake ni ya muda mrefu, kama sumu. Namna yoyote ya msingizio, maongo yenye chuki, matisho ya hadhari, ugomvi wa uchungu, kulaani kwa makusudi, kudanganya tegemeo la mtu au hata dhihaka, zote hizo ni za kuua kiroho. Kwanza zinatia sumu moyoni mwa yule anayetamka maneno kama hayo, ndipo zinatia sumu kwenye akili ya mtu anayeshambuliwa. Yesu alisema, „Yeyote aliye na hasira juu ya ndugu yake bila sababu itampasa kuhukumiwa. Na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto“ (Mathayo 5:22). Kwa njia ya tamko hilo Yesu alitueleza sisi sote kwamba tu wenye makosa na kutuhukumu kuwa wenye mioyo ya uovu na wenye roho ya uuaji, tunaostahili jehanum.

Tunahitaji kuungama na kukiri kwamba, wote tunao mawazo ya ki-uaji mioyoni mwetu. Hasira, wivu, kuning’inia katika mahojiano ya chuki, roho ya kutaka kulipiza, ukatili na ukorofi ndiyo tabia na matendo yanayowasumbua watu na sio wazima tu, hata na watoto. Si ajabu kwamba Yohana asema, “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji”(I.Yohana 3:15) Tunatakiwa kujipima wenyewe kwa uaminifu, ili tutambue, kama tunajisikia kuwa na chuki dhidi ya mtu; ndipo tutahitaji kumwomba Mungu tushinde chuki yetu kabisa. La, sivyo, mawazo hayo mabaya yanaweza kuota mizizi ndani ya mioyo yetu na kutupotosha. - Yesu anamtazamia kila mtu anayekariri Sala ya Bwana kwamba, amsamehe mtu yeyote kabisa, jinsi Mungu alivyosamehe makosa yetu yote. Daima Mungu atutazamia tusamehe. Kutaka kwetu kusamehe kutatusaidia kushinda, na uamuzi wetu wa kusamehe utashinda hata na hamu yetu ya kuangamiza adui zetu.. - Basi yawezekana unakubali kumsamehe adui wako, lakini bado huwezi kusahau tendo lake baya. Haya, uwe mwangalifu! Kama ni hivyo, yawezekana tunamwuliza Mungu atusamehe dhambi zetu, lakini asiyasahau makosa yetu. Au pengine tutasema, “Niko tayari kusamehe dhambi ya rafiki yangu na kusahau tendo lake ovu dhidi yangu, lakini sitaki kumwona tena kabisa!” Je, unataka kuja kwake Mungu, lakini usikutane naye tena wala kumwona ? Unataka akutendee sawasawa na jinsi unavyomtendea adui yako?

Yesu alituachia njia moja tu ya kupata na kutunza amani, jinsi alivyosema, „Wapende adui zako. Wabariki wale wanaokulaani. Uwatendee mema wale wanaokuchukia, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni“ (Mathayo 5:44-45). Hatuwezi kushinda chuki yetu isipokuwa kwa nguvu ya upendo takatifu unaotulia ndani ya waumini wenye mioyo ya kupondeka. Kwa sababu hiyo, Yesu bila mashaka yoyote atuonya: „Msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu (Matyayo 6:15).

Haya, kwa nini Wakristo wanaweza kuwasamehe adui zao makosa yao yote, wakati kila mkosefu anastahili kuadhibiwa? Kufanya hivyo isiyo haki, je, haitalia hata mbinguni? Basi, ni kweli! Mungu hawezi kuachilia dhambi yoyote bila adhabu, jinsi ilivyoandikwa, “Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi.“ (Waebrania 9:22b). Kwa sababu hiyo Yesu alibeba dhambi zetu na kubeba adhabu kwa niaba yetu. Neno la Mungu lasema, „Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.(Isaya 53:5). Yesu, Mwana wa Mungu, alibeba dhambi zetu za binafsi, pia na dhambi za wafanya dhihaka wote na wauaji. Ndiyo sababu sisi nasi tunayo faida ya kuweza kusamehe makosa ya yeyote bila matazamio. Sasa hatuna sababu tena kutafuta haki au ulazima wa kuchunguza yaliyo sawa kwa njia ya kulipa maovu kwa maovu. Katika kuteswa kwake na kufa badala yetu Yesu alitimiza mahitaji yote ya haki tukufu. Yeye ndiye amani yetu. Yeyote aendeleaye kupigania haki yake na kutafuta uadilifu kwa ajili yake mwenyewe, basi anajihukumu mwenyewe. Undani yetu sisi wafuasi wake pendo pekee ndiyo utimilifu wa sheria. Kujizuia na upendo kunamaanisha kujiweka chini ya hukumu tena. Yesu pekee huumba tabia mpya na kutaka kwetu kuwa mpya pia na kutusaidia kusamehe jinsi anavyosamehe Mungu.


08.4 - Dini ya Upanga

Watu wote wanaotambua habari ya neema ya msamaha anautoa Yesu, basi watachukizwa kuona Uislamu unavyoamuru kwamba, watu watafute kisasi kwa kumwaga damu. Vita takatifu (Jihad) ya kuua kwa kusudi ni agizo takatifu ya kiislamu. Uislamu unaruhusu kuua kwa ajili ya dini na kufanya tendo hilo kuwa wajibu kwa Mwislamu. Mhamadi aliandika ndani ya Kurani, „Wachukue na kuwaua kote utakapowakuta“, na pia, „usichague rafiki wala msaidizi toka kwao“(Suras al-Nisa 4:89,91 au al-Baqara 2:191). Roho wa Kristo hawezi kusena kwa njia ya maneno kama hayo, bali ni roho wa yule „mwuaji tangu mwanzo“.

Mhamadi aliwaua adui zake wenyewe mmoja mmoja, na yeye binafsi alijiunga na mashambulio 27. Kwa kweli aliagiza kaburi la jumla lichimbwe kwa ajili ya Wayahudi walioishi Medina, ambao aliwashitaki fitina wakati wa vita ya Khandaq.

Tangu vita ile ya Badr, Waislamu wote wanaoua adui zao katika vita takatifu wanahesabiwa haki kwa maneno ya Mhamadi aliposema, „Wewe hukuwaua, lakini Allah aliwaua. Wewe hukupiga bunduki ulipopiga, lakini Allah alipiga“(Sura al-Anfal8:17). Waislamu wa kiasi hawathibitishi maelezo ya mstari huu wa Kurani, lakini watishi wa kidini wanayatumia, ili kujisafisha mbele ya baraza. Mafunuo ya Mhamadi yalitolea thibitisho la haki kwa ajili ya kila mwuuaji wakati wa vita takatifu. Na zaidi ya hapo, yeyote anayekufa ndani ya vita ya Kiislamu dhidi ya kafiri, anaenda paradiso moja kwa moja, ambapo starehe zisizoweza kuelezwa na za tamaa za kimwili zinamngojea. Upande wa pili, Mwislamu haruhusiwe kumwua Mwislamu mwingine kwa kusudi, kwa sababu kuua namna hii ni dhambi isioweza kusamehewa kufuatana na sheria ya kiislamu. Lakini waabudu sanamu na wote wasio Waislamu hawajaliwi ulinzi wowote. Kuwaua wapagani kunahesabiwa kuwa tendo jema na kumpatia mwuaji jawabu njema za mbinguni.

Katika sheria ya Kiislamu tunakuta mpangilio wa haki iliyo ya kigeni sana kwetu. Malipo ya juu, yaani damu iliyo mwagwa, al-dyia, inaweza kuwa badala ya kisasi. Lakini hata kwenye ajali ya gari, sheria ya jicho kwa jicho, jino kwa jino hutumika, ikiwa ni halali au sio halali, ndani ya nchi zinazotumia sheria ya kiislamu. Ni vigumu kabisa kufikia suluhisho, kwa vile haki ya kiislamu inatumia namna ya pekee ya malipo, inayodai kweli na haki zitumike bila huruma. Waislamu hawana badilisho, au Mwana Kondoo wa Mungu aliyetengeneza ukombozi wa daima. Hawajui kabisa neema ya Mungu iliyoshinda madai ya kweli au haki. Hivyo inawapasa kutimiza sheria bila huruma.


08.5 - Hotuba ya Mlimani inapinga Jihad

Maisha wakati wa Agano la Kale iliwekwa juu ya msingi wa haki au uadilifu. Amri za Musa zilienea kwenye kila sehemu ya maisha, wala si amri kuhusu maisha ya binafsi, bali pia kuhusu taratibu za kidini. Hivyo mamlaka ya kidini ya serikali yao ilikuwa ya lazima kwa kuhimiza malipo ya adhabu kwa ajili ya kuvunja amri au sheria. Vita ya kidini ni tukio isiyokwepeka katika Agano la Kale na ufahamu wa sheria na serikali upande wa kiislamu. Lakini tangu Yesu Kristo alipohubiri kwamba, kila mtu na ampende hata adui zake, naye akaishi hivyo; basi vita zote za kidini zimepoteza uhalali wake. Vita za Wakristi kuelekea Nchi Takatifu, hasa Yerusalemu, zilikuwa dhambi, pia zlikuwa hatua ya kurudi nyuma katika uhusiano wa dini na mamlaka ya kisiasa. Yesu hakuwatuma mitume wake ndani ya ulimwengu kuhubiri Injili hali wamejipamba na mapanga. Kinyume cha hayo, Yeye alisema kwake Petro, „Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga“ (Mathayo 26:52). Yesu bila kujizuia alienda hadi msalabani akafa, iwapo alikuwa bila hatia yoyote, naye alikataa kuwaangamiza adui zake na jeshi la malaika. Roho wa Kristo ni kinyume kabisa dhidi ya roho wa Mhamadi. Yesu alihubiri katika hotuba yake ya mlimani, „Mmesikia kwamba imenenwa, jicho kwa jicho na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kuume, mgeuzie na la pili“ (Mathayo 5:38+39). Hivyo basi Yesu alishinda njia ya zamani, iliyodai haki ya kujipigania mwenyewe. Udhaifu wa kimwili wa Kristo katika kusulibiwa kwake pamoja na enzi yake ya upendo, imani na tumaini zilikuwa ndiyo njia ya pekee kumshinda Shetani na pia kutimiza kabisa madai yote ya amri takatifu.

Mkristo anakabili swali la kuchagua: Nitafanya nini nikitengwa kwenda huduma ya jeshi na kutakiwa kutumia silaha za kisasa ndipo pengine baadaye kupigania katika vita? Hii inamaanisha kwa ajili ya raia anayeamini katika taifa kubwa, au pia kwa mwanachama wa kundi ndogo la kikristo katika nchi isiyo ya kikristo? Katika hatua mbalimbali za historia waumini tofauti-tofauti pia walikuwa na majibu yaliyoachana katika maswali hayo magumu. Ndugu fulani walikuwa tayari kutupwa magerezani kwa ajili ya makusudi yao ya amani na hata kufa kama mfia dini kwa ajili ya Kristo. Wengine walitaka kuwa watiifu kwa mamlaka iliyowekwa juu yao na Mungu. Wao waliona sheria dhidi ya kuua kuwa ni jambo la binafsi


08.6 - Wauaji wa Kisasa

Hotuba ya Mlimani, ambayo ndani yake kuna maelezo juu ya ufalme iliyo chini ya agano jipya, itaweza kufanya kazi tu katika masingira ya binafsi ya mtu. Inaonekana kwamba, bado si wakati wake kuitumia kisiasa. Mtu anapojitokeza kijeuri kutaka kufanya Amani, basi inaonyesha kwamba, hajaelewa kabisa Hotuba ya Mlimani, yuko sawa na wale ambao kutokana na makusudi ya huruma ya kibinadamu isiyo sawa, na hivyo kutetea tendo la kuharibu mimba kote ulimwenguni. Maana hii ndiyo tendo la kuvunja sheria kubwa ajabu inayotendeka katika historia. Mamilioni ya mimba hai zinauawa ndani ya tumbo la uzazi. Wakina mama na baba wengi wanabeba kamba ya uuaji kwenye dhamiri zao. Tunaishi katika kizazi cha wauaji nasi bila kujitambua tu sehemu ya kizazi hicho.

Makumi elfu ya watu wanahusika na ajali za magari, si kwa ajili ya bahati mbaya tu au kwa sababu ya teknologia ya kisasa, lakini kwa sababu ya kulewa, kuendesha haraka kupitiliza vipimo vya upesi au hata kwa uchovu. Tukitaka kweli kushika amri ya sita, twahitaji kuhesabia ajali za magari kuwa mauaji, na hivyo kwa bidii sana kubadilisha tabia ya kuendesha magari yetu. Twahitaji kuziendesha kwa kujitawala kwa tabia ya unyenyekevu, tukitafuta sana ulinzi wa Mungu na kumwomba sana atupatie subira.

Twaishi katita wakati wa kuchafua mazingira yetu, hata hewa; maji na vyakula vyaweza kuwa na sumu. Labda masumbufu hayo ya Mungu yaweza kupunguzwa, tukihifadhi mazingira yanayotuzunguka, pia na kuinua macho yetu kwa Mungu, tukimwomba atuonyeshe namna ya kuishi sawa. Kwa njia hiyo tu twaweza kutunza ulimwengu wetu bila kuhangaika namna ya kuuharibu sisi wenyewe.

Kuzidisha chakula ni njia inayojificha ya kujiua mwenyewe, na maelfu ya watu wa jamii yetu ya kupenda anasa wanaifuata, na hivyo kujiua polepole. Wengine wajiingiza katika matumizi mabaya ya kutwaana na hivyo kuharibu miili yao, roho zao na mioyo yao. Yeyote aliye na uchoyo au umimi atapatwa na unyogovu na upweke, ambazo pia zaweza kupunguza maisha. Pia na kuchapa kazi kwa kuzidisha, bila kutulia na kupumzia, au mazoea mabaye, yote ni kujiharibu mwenyewe. Kulala bila taratibu na kuishi ovyo ndiyo dhambi dhidi ya mwili wako mwenyewe, kwa sababu tu mali ya Mungu, wala si mali yetu sisi wenyewe.

Yesu alitufundisha kujikana wala si ukinaifu aliposema, “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona”(Mathayo16:25). Paulo akakaza hilo akisema, “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu”(Warumi 14:17). Maisha ya kiroho ya taratibu yatatokeza maisha ya kimwili ya taratibu na yanaandamana na amani ya moyo na akili.

Amri ya sita inakataza namna yoyote ya uuaji, na pamoja na hayo inatutia moyo kukazana katika kutenda matendo ya upendo. Inajaribu kuamsha huruma ndani yetu kwa ajili ya wale wanaoishi katika umaskini. Tusimpite mhitaji kana kwamba hatumwoni, lakini tuchukue muda naye na kumsaidia kiasi kinachowezekana. Yesu, aliye upendo wa Mungu ulioingia mwilini, alituonyesha, namna ya kuifanyia kazi agizo hilo kwa matendo maishani mwetu. Roho yake atatuongoza tukimwuliza atupatie hekima. Ni Yesu tu awezaye kugeuza hata wauaji wawe watoto wa upendo wake na atawasaidia kuwaokoa waliopotea wapone kiroho nao. Jambo hilo litatendeka tonapowaelekeza kwa yule Mganga aliye Mkuu wa waganga wote, Yesu, awezaye kuwafanya wawe wapaya na watakatifu kutoka ndani na kubadilisha utu wa ndani ulio wa ki-uaji uwe utu wa kuhudumia na kupenda.

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:56 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)