Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 117 (Jesus appears to Mary Magdalene)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)
1. Matukio siku ya Pasaka asubuhi (Yohana 20:1–10)

c) Yesu anamtokea Mariamu Magdalene (Yohana 20:11–18)


Yohana 20:11-13
„Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo alipolazwa mwili wake Yesu. Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.“

Wale wanafunzi wawili walirudi baada ya kuhakikisha kwamba kaburi ni tupu. Hawakuona sababu ya kubaki.

Hata hivyo, Mariamu Magdalene alirudi kaburini baada ya kuwaambia wanafunzi kwamba imekuwa tupu. Aliendelea kubaki, ingawa hao wawili walirudi nyumbani, maana hakuridhika na hali hiyo kwamba mwili umetoweka. Alitamani kuendelea naye, maana yeye alikuwa ni tumaini la nguvu yake. Kupotelewa na huo mwili, tumaini lake lilianza kuyeyuka. Akabaki na kulia kwa uchungu.

Ndani ya kina kirefu cha huzuni yake, Yesu akamtumia malaika wawili ambao waliwatokea na wale wanawake wengine nao. Hapo aliwaona wakikaa kwenye kaburi tupu katika nguo nyeupe zilizutia nuru ndani ya huzuni. Lakini hawakuweza kumfariji hasa, maana kumwona Yesu kipekee angefarijika. Moyo wake ukalia, „Uko wapi, Bwana wangu?“

Wito huo nyamavu unatuelekea sisi. Tunataka nini sisi? Kwa nani tunataka yale tunayoyatamani? Zipi ni shabaha zetu? Tuko tunaambatana na Magdalene kimawazo tusitake chochote, ila kumwona Yesu tu? Je, mioyo yetu inalia kwa kutamani arudi tena?

Yohana 20:14-16
“Naye akiisha kusema hayo akageuka nyuma, akamwono Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).”

Yesu aliitika kwa mlio wake. Wakati wengine walitamani kuona kaburi wazi na kusikia malaika, Mariamu Magdalene alitazamia kupata maono; Yeye tu ! Na Yesu akamtokea, akisimama mbele zake, kama mtu wa kawaida , bila duara ya nuru kichwani.

Alikuwa amehuzunishwa mno, hakutambua sauti ya Yesu, wala hakusikia malaika. Alitamani tu kumwona Yesu, sio kusikia maneno yake tu. Hata hivyo alishindwa kutambua kuwepo kwake dakika hiyo, kwa sababu moyo unaohuzunika unakosa kutambua kuwepo kwake Kristo; ni hivyo hata kwetu, na tutashindwa kusikia maneno yake ya kutuliza. Hivyo wengi wanaomtafuta Mungu Mwumbaji hawampati, maana wanatamani kutafuta-tafuta tu na kuuliza-uliza badala ya kumwona Mchungaji atafutaye.

Lakini Yesu alielewa upendo wa Mariamu, naye akavunja vizuizi vya kukata tamaa kwake kwa maneno yake ya huruma; alimwita kwa jina lake, akafunua kwamba yeye ni zaidi ya mwanadamu, wala si mtunza bustani. Yeye ndiye ajuaye yote, mwenye hekima, ndiye Bwana mwenyewe. Alimwita Mariamu jinsi Mchungaji Mwema awaitavyo kondoo yake, amjuaye hata kwa jina, akimtolea uzima wa milele. – Yeyote ampendaye Yesu atatambua upendo wake na kupokea msamaha wa dhambi zake wakati Bwana anapomwita kwa jina, akimjalia na faraja ya Roho Mtakatifu.

Yesu wakati huu anakuita kwa jina na wewe. Unasikia sauti yake, ukiacha nyuma mashaka yako yote, pia na dhambi, ukimjia?

Mariamu akaitika kwa neno moja, “Bwana!” Neno ambalo Mariamu alilitumia (Raboni) Maana yake ni mmoja ajuaye yote na kuwa mwenye enzi yote. Akawa na mapendeleo kuwa mwanafunzi katika shule yake, naye akamjalia ufahamu wake, nguvu, ulinzi na uzima wa milele. Basi jibu lake likajumlisha kipeo cha furaha ya Kanisa linalomngojea, ambalo baada ya matazamio ya muda mrefu litamwona Bwana wake akija katika mawingu, likimwabudu katika utii na kumtukuza na Halleluya tele.

Sala: Bwana Yesu, tuna inama mbele zako kwa ajili ya kuitika kwako kwa hamu ya Mariamu ukimtokea wazi. Ulimfariji kwa kuwepo kwako karibu naye. Neno lako ndilo uzima. Twaomba ufungue masikio na mioyo yetu ili tupokee maneno yako. Utujalie utii wa kukutegemea kabisa kwa furaha.

Swali 121: Kwa nini Mariamu hakuacha kutafuta mwili wa Bwana Yesu, mpaka alipojifunua mwenyewe kwake, akimwita kwa jina lake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 25, 2017, at 02:57 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)