Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 096 (The Holy Spirit reveals history's developments)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

4. Roho Mtakatifu hufunua maendeleo ya ajabu kabisa katika historia (Yohana 16:4-15)


YOHANA 16:4-7
“Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi. Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmojawenu aniulizaye, Unakwendapi? Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.”

Mwanzoni Yesu hakujadili na wanafunzi wake habari ya magumu, maumivu na mateso watakaoweza kupata, bali aliwajulisha jinsi mbingu ilivyopata kufunguka na malaika kupaa na kutelemka juu ya Mwana wa Adamu. Walifurahia katika kutambua nguvu ya Mungu ikifanya kazi ndani ya Mwana hata kutenda miujiza mingi. Pole pole hao washupavu walikaza shabaha zao dhidi yake, na makutano ya watu wakatengana naye kwa hofu ya Wayahudi. Hakuna aliyesalia ila hao wanafunzi wake tu, ambao sasa ilipasa awaache, yeye akirudi kwa Baba yake mbinguni. Hapo tu alianza kusema habari ya mateso na kifo, na wao wakazidi kushikwa na huzuni. Walishindwa kutambua shabaha au maana, ambayo hapo mbeleni ingeweza kuwatia matumaini. Lakini waliona kwamba Yesu hakusema lolote kuhusu maumivu yake mwenyewe, wala kuhusu mateso makali na kifo; aliongea tu habari ya kuondoka kwake kwenda kwa Baba, akitumia maneno ya kutia moyo. Wakamwuliza, “Unakwenda wapi?” Hawakutaka kumwona akipaa mbinguni, bali walitamani aendelee kukaa nao. Yesu aliwajibu kwa uwazi kabisa kwamba ni lazima kwake kuwaacha, maana bila msalaba hata Roho Mtakatifu asingemwagwa kwao. Kipekee kwa ajili ya upatanisho wa Mungu na wanadamu, na kule kufutwa dhambi kwa njia ya kifo cha Mwana Kondoo wa Mungu mahali petu, akiba kuu ya enzi ya Mungu ilifunguka na kuwajalia wafuasi wake. Yesu alitimiza kikamilifu haki zote zilizotakika, ili uhai na upendo wa Mungu kuweza kumwagwa juu yao. Kifo cha Yesu ndiyo msingi wa Agano Jipya, na inakupatia haki ya kushirikiana na Mungu. Roho Mtakatifu ndiye yeye ayatokezaye hayo yote na kukufariji, akikuhakikishia kwamba Mungu yu pamoja nawe na kuishi ndani yako.

YOHANA 16:8-11
“Naye akiisha kuja huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.”

Roho aweza kuwa fariji wanafunzi, kwa sababu awafungulia macho ya waumini, naye ahukumu mioyo ya wasioamini kwa msingi wa kanuni hizo.

Roho Mtakatifu hutufundisha maana ya dhambi na mwisho wake. Kabla ya kuja kwake Kristo, dhambi ilikuwa tendo la kuvuka mipaka ya maagizo ya torati, na pia ilikuwa jambo la kukosa kutimiza mapenzi ya Mungu. Hii inahesabiwa kuwa ni maasi na upungufu wa tumaini na upendo - ni maisha bila Mungu na kinyume chake. Dhambi zote, zikiwa za maadili, za kijamii au za kiroho, zote zilihesabiwa kuwa ujeuri dhidi ya enzi ya Mungu. Baada ya msalaba wa Yesu, maana hizo zilijumlishwa katika moja inayotendeka na mwanadamu, nayo ni kumkataa Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa binafsi - au kwa maneno mengine ni kukataa neema ya bure ya Mungu. Yeyote atakayedharau neema ya Yesu, anamtukana huyu Mtakatifu, na yule asiyekubali kumwamini Mungu kuwa Baba na Yesu Mwanawe atakuwa adui wa Utatu Utakatifu. Mungu ni pendo, na yeyote akataaye huo upendo unaodhihirishwa ndani ya Kristo, anatenda dhambi ya kifo inayomtenga na wokovu.

Msalabani Kristo alikamilisha wokovu wa ulimwengu mzima. Hahitaji kufa tena, kwa sababu aliwasamehe wanadamu wote dhambi zao zote, wawe wenye umri yoyote ile. Wote wanahesabiwa haki kwa neema katika damu ya Kristo. Hivyo yeye amekuwa Kuhani Mkuu, na huduma yake inajumlisha hatua tatu: Kwanza kupigwa kwake yeye aliyeuawa (Yesu). La pili, kutoa sadaka ya damu yake kwa Mtakatifu wa Watakatifu, inayomaanisha kukamilisha malipo(kafara) mbele za Mungu. La tatu, ni kutoa baraka kwa mamilioni ya waumini wanaoingojea. Hayo yote Yesu aliyatenda. Kwa sadaka hiyo alimwaga baraka ya Roho Mtakatifu, ili atuhakikishie kwamba sasa tunahesabiwa haki. Ufufuo na kupaa kwake Kristo mbinguni yanakamilisha thibitisho kwetu iliyoanzishwa msalabani.

Yesu hakuona shabaha ya ulimwengu kuhukumiwa kama jambo tu la kutupwa kwa wasioamini ndani ya moto wa jehanum, lakini pia anaona kamilisho la hukumu hiyo katika kumharibu Shetani na utumwa wake. Yule ndiye anayewavuta wanadamu mbali na ushirikiano na upendo wa Mungu. Aliwafunga ndani ya minyororo ya chuki, akiwafanya kuwa watoto wa ibilisi wakijaa na madhumuni ya kuchanganya mambo. Yesu katika maisha yake ya hapa duniani na kutembea kwake katika unyenyekevu alihukumu kiburi cha huyu mwovu. Upendo wa Mwana ulimwondolea silaha zote yule Mwovu. Wakati Yesu alipokabidhi roho yake mikononi mwa Baba yake msalabani, ndipo aliposhinda giza linaloenezwa na Shetani. Yesu ndiye Mshindi, mbali na udhaifu wake uliyoweza kuonekana. Uaminifu wake hadi kifoni ilikuwa ni hukumu juu ya Shetani na kumshinda kabisa. - Sisi twaishi kwa wakati ambapo ushindi huo unaendelea kufanya kazi. Tunaomba kwake Baba: “Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu”, tunapotambua matokeo ya ushindi wa Kristo katika kulindwa na maovu, pia na hakika ya ushindi maishani mwetu.

SALA: Asante sana, Bwana Yesu, kwa sababu ulivipiga vita vilivyo vyema, na ulidumu katika uaminifu na unyenyekevu, upendo na tumaini. Tunakushukuru pia, kwamba ulimwendea Baba ukakamilisha kupewa haki kwetu. Tunakuhimidi na kukusifu na “Halleluya” mara nyingi, kwa sababu uliweka baraka za sadaka yako ndani yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Ututunze ndani ya upendo wa uadilifu wako, hata adui yule asiweze kupata nafasi ya kushinda juu yetu. Tuokoe na Shetani, ili ufalme wako uweze kukaribia, na hata jina la Baba yako lipate kutakaswa duniani kote.

SWALI:

  1. Roho Mtakatifu hufanya kazi gani humu ulimwenguni?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:50 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)