Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 090 (Abiding in Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

1. Kudumu ndani ya Kristo kunaleta matunda mengi (Yohana 15:1-8)


YOHANA 15:1-2
“Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.”

Yesu baada ya chakula cha jioni alishuka pamoja na wanafunzi wake kutoka Mlima Mtakatifu, akipita milango ya kuta za jiji upande wa bonde la mto Kidroni, ndipo wakapanda kuelekea mlima wa mizeituni wakipita kati ya mashamba ya mizabibu. Wakitembea hivyo, Yesu alieleza zaidi maana ya imani kwa wanafunzi wake na pia kusudi la upendo wao, akitumia mzabibu kuwa kielelezo.

Yesu alimweleza Mungu Baba kuwa ndiye mkulima wa mzabibu, aliyepanda mizabibu kote ulimwenguni. Mmojawapo kuwa ni watu wa Agano la Kale, jinsi tusomavyo katika Zaburi 80:8-16, pia na kwa Isaya 5:1-7. Mungu hakupendezwa na mzabibu huo, kwa vile haukuleta matunda mema. Basi Mungu akapanda mche mpya kwenye ardhi, ambaye ni Mwana wake, aliyezaliwa na Roho, ili yeye awe ndiye mzabibu wa kweli atakayeleta aina mpya ya mzao mpya utakaokuwa na furaha ya kuleta matunda ya kiroho, tena tele. Jambo hasa ambalo Yesu alilowadokezea wanafunzi wake ilikuwa ni kuleta matunda ya Roho Mtakatifu kwa unyenyekevu, matunda ya thamani ya aina mbalimbali ya kiroho. Alifahamu kwamba mafundisho ya kibinadamu kwa vyovyote yaweza kuwa na makosa. - Aina ya mnyama huishi ndani ya mwanadamu, anayongojea nafasi ya kuchokozwa, ili akanyage wengine na kuwameza. Yesu alitamka hayo mapema katika mafundisho yake, kwamba yeye pekee aleta matunda yanayokubalika mbele za Mungu, naye ndiye mleta amani na mjenzi wa Kanisa, ambalo ni tunda hasa.

Katika mfano wakeYesu kwanza alionyesha upande usiofaa, kwamba yule asiyejifungua kwa msukumo wa upendo, wala kuleta matunda ya kiroho na kukataa kuruhusu mtiririko wa maji ya matunda ya mzabibu - Mungu atamkata na kumwondoa kwenye mzabibu kama tawi lisilofaa. Mungu asipoona matunda ya Injili ndani yako, au asipoona namna ya kifo cha Kristo na kufufuka kwake ndani yako kama matengenezo na tokezo toka kwake, basi atakukata kutoka kwa mzabibu huyu Mwana wake.

Hata hivyo, mara atakapoona maji ya matunda ya Roho Mtakatifu, ataimarisha dalili hizo za kukua ndani yako, ili uwe tawi la kufaa ndani ya mzabibu. Tawi litaleta kwanza majani, halafu uzao tele. - Mungu aliye Mkulima atakata sehemu zile zisizofaa, ili uweze kuzaa matunda zaidi. Tena matunda hayo sio ya kwako, lakini ya Kristo ndani yako. Hivihivi sisi sote tu watumishi tusiofaa; Yeye ndiyo yote katika mambo yote. Je, unafahamu kwamba mzabibu unahitaji kukatwa kila mwaka wakati wake, ili uweze kuleta matunda safi mwakani? Mungu naye huondoa kwa kukata yote yasiofaa ya kibinadamu, ili kutokufaa kwako kupate kwisha, nawe ufe kwa dhambi. Na hivyo tu uhai wa Kristo ndani yako utachujwa ili upata hali ya kukomaa. Bwana anayo njia nyingi kukuokoa kutoka kwa utu wako wa ubinafsi. Mambo, makosa na maharibiko yatakushambulia ili uvunjike. Usiishi kwa ajili yako mwenyewe, lakini ndani ya Bwana; hivyo utakuwa mtu wa kupendeza kwa njia ya nguvu zake.

YOHANA 15:3-4
“Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.”

Yesu huleta faraja juu yenu. Mungu hataki kukukata katika mzabibu kwa sababu ya ubovu wetu wa asili na makosa mengi. Yesu alitutolea kila mmoja wetu hatua ya kutusafisha kikamilifu hapo mwanzoni, akitutwisha hilo wakati tulipokata shauri ya kumwamini. Usije ukasema, “Hapo baadaye tutasafishwa kwa kumtumikia Mungu na kumwomba.” Tayari alitusafisha kwa kila namna; yeye ndiye aliyetusamehe mara moja kwa ajili ya yote na kututakasa kule msalabani. Injili inatokeza nguvu ya usafisho. Hivyo sio bidii zetu, wala kuteseka kwetu au kukomaa kwetu kunayotutakasa, bali ni Neno la Mungu pekee. Jinsi Mwumbaji alivyotokeza ulimwengu hapo mwanzo kwa Neno moja, ndivyo naye Kristo aliumba usafi ndani yetu, mara tulipojifungua kwa Neno lake. Sio tendo la ubatizo au kushiriki chakula cha Bwana yanayotusafisha, bali ni imani ndani ya Neno la Yesu, ndipo kulitafakari mchana na usiku. - Basi soma fungu fulani katika Biblia kila siku, bora ujizoeze kwa saa fulani kila mara; la sivyo, bila kutumia chakula cha kiroho, utaanguka.

Yesu alikaza neno moja, ambalo ndani yake kukua kwetu na kuzaa matunda mengi linategemea. Neno hilo ni KUDUMU . Neno hilo latokea mara kumi kwenye sura ya 15 ya Yohana. Maana nyingi zinaweza kuelezwa na tamko hilo - sisi tunadumu ndani yake na yeye ndani yetu; tunatakaswa katika hatua za kudumu; nguvu na maji ya matunda hudumu kutiririka kupitia kwetu. Mambo mema yote yatoka kwake, hivyo tunapasa kudumu ndani yake. Ikiwa tunaondoka kwake, ndipa mtiririko wa nguvu ya upendo wake hukoma ndani yetu. Kama tawi linavunjika kutoka kwake, hata kama ni kwa muda mfupi tu, basi itakauka. Basi tu, jinsi ilivyo picha mbaya kwa kanisa likikauka na kufa! Sala muhimu sana kabisa kwa mwumini ni kuomba kudumu ndani yake. Ili kwa njia hiyo Bwana aweze kufanya kazi ndani yetu kila wakati kwa kutukuza, kuleta matunda na utendaji wema; na hivyo atudumishe ndani ya jina lake usiku na mchana. Kudumu basi sio uwezo wetu, bali ni neema toka kwa Roho Mtakatifu. Hakuna awezaye kudumu ndani ya Kristo peke yake, lakini twaweza kumshukuru kwa zawadi hilo, na kumsihi atutunze katika kudumu ndani yake; na watu wengine nao wapate kudumu ndani yake pia.

SALA: Bwana Yesu, wewe ndiwe Mzabibu mtakatifu wa Mungu ndani ya ardhi ya dunia yetu. Toka kwako tunapokea makusudi yote mema. Mioyo yetu ni asili ya maovu yote. Tunakushukuru kwa sababu ulitusafisha kwa njia ya Injili. Ututunze ndani ya jina lako, ili nguvu ya Roho yako Mtakatifu atokeze tunda la upendo na la kudumu. Bila wewe hatuwezi lolote. Imarisha huduma ya kuwaokoa ndugu zetu, wasiishi kwa ajili yao wenyewe katika udhaifu, bali waweze kudumu ndani yako.

SWALI:

  1. Jinsi gani Yesu alipata kuwa Mzabibu wa kweli?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:44 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)