Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 078 (The Greeks seek Jesus' acquaintance)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
A - Utangulizi kwa Juma Takatifu (Yohana 11:55 - 12:50)

3. Wayunani walitafuta kumfahamu Yesu (Yohana 12:20-26)


YOHANA 12:20-24
“Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kenda kuabudu kwenye sikukuu. Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida wa Galilaya, wakamwomba wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. Filipo akaenda , akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu. Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu. Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.”

Wayunani walioongoka kwa dini ya kiyahudi walikutanika Yerusalemu; wao nao walikuja kwa Pasaka kutoka kwa ulimwengu wa kiyunani. Makutano walipomkaribisha Yesu kwa uchangamfu kama Mfalme, hao Wayunani nao walivutika. Basi wakaona vema wamfahamu zaidi. Hamu ya mataifa ilikuwa imejumlishwa katika swali hilo. Kwa kutambua kwamba Filipo alisema kiyunani, akakubali na kumwendea mwenzake Andrea kwa niaba yao. Ndipo wanafunzi hao wawili wakamwelekea Yesu, wakiguswa sana kwa kuona tunda la kwanza katika wale waliomjia Yesu kutoka kwa mataifa. Na pengine walijisikia hivyo kwa uwezekana wa kukimbilia nchi za Wayunani, ambapo pangekuwa na njia kwamba watoke kwenye hatari iliyowazingira hapo katikati ya Wayahudi washupavu.

Yesu alitambua mawazo yao, jinsi alivyounganisha pia hamu ya mataifa kwa njia ya ulizo waliotoa hao Wayunani. Akatoa wito wa msingi, ambalo halikueleweka wazi nao, hata hivyo kuwa ni wito wa ushindi, na likawa ni lengo kuu la injili ya Yohana: “Sasa Mwana wa Adamu hutukuzwa.” - Saa ilikuwa imekaribia kwake akuzwe, na kitambo kilichotazamiwa na mbingu na nchi kilikuwa kinakaribia.

Hata hivyo, mwujiza juu ya miujiza; ushindi katika vita, kushika nguvu ya kisiasa hazikuwa dalili za ushindi wa Yesu.Yohana hakueleza katika injili yake habari ya kugeuka sura yake juu ya mlima, maana hakuhesabu jambo hilo kuwa ni la msingi kuhusu utukufu wake. Anataja tu uhusiano kati ya kutukuzwa kwake na kifo chake. Pale msalabani twaweza kuona kiini cha uungu wake, ambacho ni u p e n d o .

Yesu alijifananisha na punje la ngano, mbegu toka mbinguni iliyodondoka ardhini, ili ajitolee kabisa na kuonyesha haki na utukufu. Yesu alikuwa na utukufu daima. Kifo chake chatutakasa sisi, tulio waasi, ili tuweze kustahili kushirikishwa enzi yake. Kufika kwa Wayunani kulitokeza wito wa shangwe, kwa sababu kulionyesha kwamba anawaita na watu kutoka kwa kila taifa. Atafanya kwa upya ndani yao utukufu wake wa awali. Na utukufu huo utapenya ndani ya uumbaji wote na ulimwenguni kote kwa njia ya msalaba tu.

YOHANA 12:25-26
“Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu, ataisalimisha hata uzima wa milele. Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.”

Yesu atuonyesha kwamba, njia yake ya kupitia kifo na kuelekea kwenye utukufu, hata kwa wanafunzi wake itakuwa hivyo. Jinsi Mwana alivyotoka kwenye utukufu wake, akajitvua kabisa na hali yake yote ya kimungu kwa ajili ya kuokoa binadamu, ndivyo hata shabaha yetu haitakuwa ya kujikuza au kusifiwa, lakini kujikana wakati wowote. - Basi ndugu, ujipime mwenyewe, unajipenda au kujichukia mwenyewe? Kristo anasema kwamba, kama unajisahau mwenyewe kwa ajili ya kuitumikia ufalme wake kwa uaminifu utapokea uhai wa kimungu. Utasalimisha roho yako kwa uzima wa milele. Kwa maneno haya Yesu akuonyesha mkataba wa utukufu wa kweli. Usiishi kwa kupendezesha tamaa zako, wala usiwe mvivu au mwenye kiburi, lakini umrudie Mungu ukisikiliza maagizo yake, ukitafuta wanaoonewa na waliopotoshwa ukawahudumie, jinsi Yesu alivyojitoa kabisa kwa kuacha utukufu, akiketi mezani pamoja na wazinzi na wezi. Katika kushirikiana na watenda dhambi kama hao kwa ajili ya Injili, utukufu wa Mungu utajionyesha maishani mwako. Usijidhanie kwamba u bora kuliko wengine. Yesu pekee ataweza kukufanya uwe wazi kabisa mbele za wengine, ingawa unayo makosa. Mabadiliko kama haya yatakujia tu kwa kujikana mwenyewe.

Yesu aliweka wazi shabaha hiyo, alipoeleza kwamba huduma yetu kwa ajili yake inamaanisha kumfuata na kumwiga yeye, pia kushiriki katika kudharauliwa jinsi alivyoyavumilia mwenyewe mara kwa mara. Kanjia hiki sio kupata fahari na anasa na majivuno; hayo sio namna ambazo wafuasi wa Kristo wazitazamie. Yawezekana watapata kukatazwa, uadui na hata kuhukumiwa hadi kufa. Je, u tayari kuteseka kwa ajili ya jina lake? Mwenyewe anaahidi: “Mahali nilipo, mtumishi wangu naye atakuwapo.” Yesu alitangulia mbele yako kwenye kanjia cha usumbufu, naye avumilia pamoja nawe. Utukufu wa nje sio lengo la watumishi wa Kristo katika safari hiyo. Furaha yetu sio katika kujipendeza sisi wenyewe, lakini ni huduma kwa ajili ya wenye kuhitaji. Jina la Kristo linatukuzwa katika roho ya kujitoa ya wafuasi wake. Na jina la Baba latukuzwa, sisi tunapoendelea kufanana na Mwanaye.

Jinsi Kristo anavyoketi leo kwenye kiti cha enzi cha Babaye, akiishi naye katika ushirikiano kamili na umoja, ndivyo hata wale wanaodhulumiwa leo kwa ajili yake, wataishi na kuunganika na Baba yao wa mbinguni. Siri hii ni kubwa mno. Je, unafikirije, utakuwa na heshima hiyo ambayo Baba atatolea kwa ajili ya watumishi wa mpendwa Mwana wake? Atatengeneza sura yake ndani yao, jinsi ilivyokuwa wakati wa uumbaji. Na zaidi ya hayo, atashuka juu yao katika ukamilifu wa Roho yake. Nao watakuwa watoto jinsi alivyo Mwana wake, yeye akiwa kama mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi. Milele watakuwa pamoja na Baba yake mbinguni. (Warumi 8:29; Ufunuo 21:3-4)

SALA: Tunakushukuru, Bwana Yesu, kwa sababu hukutamani kufurahia utukufu wako pamoja na Baba, lakini ulijivua na ukuu wako wote. Tunakuabudu kwa unyenyekevu wa namna hii. Tunakuomba utuweke huru na hali ya kuridhika kwetu na kiburi chetu, ili tupate kutambua uhuru ambayo Roho yako anautoa ili tukutumikie na kutambua upendo wako maishani mwetu.

SWALI:

  1. Kwa vipi kifo cha Kristo kinaelezwa kuwa ni kutukuzwa kwa ukweli?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on September 01, 2014, at 04:31 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)