Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 063 (The Jews interrogate the healed man)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
2. Kumponya mtu aliyezaliwa kipofu (Yohana 9:1-41)

b) Wayahudi wanamhoji yule aliyeponywa (Yohana 9:13-34)


YOHANA 9:13-15
“Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani. Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho. Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.”

Maisha ya kiyahudi yalikuwa kama gereza ndani ya ma-sheria; walisumbuka zaidi kuhusu kuvunja sabato, kuliko kusikia furaha ya uponyaji. Majirani na wapelelezi walimpeleka yule mponywa kwa Mafarisayo, ili wao waamue, kama uponyaji huo ni wa Mungu au kwa wafanya kazi wa kishetani.

Hivyo yakaaanzishwa mahojiano na majadiliano kumhusu Yesu. Huyu mtu aliyeponywa alieleza jinsi uponyaji huo ulivyofanyika. Alifupisha tamko lake, kwa vile furaha yake katika kuponywa ilichafuliwa na chuki za maadui wa Yesu.

YOHANA 9:16-17
“Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki Sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa mtengano kati yao. Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.”

Baada ya kusikiliza ushuhuda wake, hao wanasheria wakaanza kuhojiana. Wengine walisema kwamba Yesu hana nguvu toka kwa Mungu, kwa vile alivunja amri ya Mungu. Hivyo wakaweka hukumu juu ya Yesu kwa hoja za kisheria.

Wengine wakaona uhusiano kati ya dhambi ya yule kipofu na kupona kwake na kusamehewa. Wakafasiri kwamba uponyaji huo lazima uwe na maana kubwa zaidi, maana ilihusika na uwezo wa Mungu wa kusamehe. Hivyo kwao haikuwezekana Yesu kuwa mwenye dhambi, maana yeye mwenyewe alisamehe dhambi na kutengeneza shida ya yule mtu.

Walishindwa kusuluhisha maoni hayo mawili. Pande zote mbili walikuwa vipofu, - sawa na watu wengi wa siku hizi, wanaojadili juu ya Yesu kiakili tu na bila hoja kamili. Basi walimhoji yule mponywa, ili wagundue kama Yesu alikuwa amesema na mengine, na jinsi alivyoona yeye kumhusu Yesu. Maulizo kama hayo yafaa kwa watu wanaofahamu mambo fulani juu ya Yesu, ni vema kuwauliza wale waliozaliwa mara ya pili. Maana hao ndio wanaofahamu namna ya kuwekwa huru na dhambi na ghadhabu ya Mungu. Mbali na hali hiyo ya kuzaliwa tena kiroho hatuwezi kumwona Mungu.

Basi mponywa akaanza kutafakari, “Yesu basi ni nani?” Alimlinganisha Yesu na watu wengine wa Mungu katika historia ya watu wake. Katika nyakati zilizopita miujiza mbalimbali ilitendeka na manabii, lakini hakuna aliyemponya mtu aliyezaliwa kipofu. Hivyo kutokana na matendo ya Yesu mtu yeyote mwenye akili angeweza kuona kwamba hapo kuna Mwokozi wa pekee. Basi huyu mtu akamwita Yesu kuwa nabii, ambaye zaidi ya kufahamu mambo yajayo, yeye naye anaamua mambo ya sasa katika uwezo wa Mungu. Yeye huchunguza mioyo na kudhihirisha mapenzi ya Mungu.

YOHANA 9:18-23
“Basi Wayahudi hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona. Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mwasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa? Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu; lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayhudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi. Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.”

Wayahudi walikataa kukiri elimu ya kuwaza kwa akili halisi kulinganisha miujiza ya Agano la Kale na kazi ya Mungu ndani ya Yesu yaliyokuwa ya kushangaza. Hawakuamini kwamba yeye ni nabii au yule Mmoja aliyetumwa na Mungu; maana wangalikubali hayo ya Yesu, msimamo wao ungalionekana kuwa na kosa nao wangalilaumiwa.

Walirudi kwenye hoja la uwongo, na matokeo yake kutamka kwamba mwujiza ule kuwa maono ya uwongo, na ya kwamba huyu mtu hakuwa kipofu kabisa. Walikuwa tayari kutaja lisilowezekana kuwa ni singizio kwamba kulitendeka mwujiza kwa mikono ya Yesu. Kumponya aliyezaliwa kipofu, kwao ilionekana kwamba haiwezekaniki, ni msiba uliotokana na hatia ya kurithiwa.

Wakaletwa wazazi wake, waliopata kusikia shida ya kijana wao na polisi. Hao wazazi walisema kwa uangalifu sana kwa ajili ya hofu kwa Mafarisayo, wakakana yale waliowahi kusikia toka kwa kijana wao. Walijitenga naye ili wasihusishwe katika taabu yake. Hivyo mwana akaachwa peke yake, ajitetee kwa ajili yake. Kufukuzwa na baraza ilikuwa ni jambo zito sana; ilimaanisha kutengwa na jamaa kama vile mwenye ukoma. Pia ilimaanisha kunyimwa haki na kufutwa nafasi ya kuoa au kuolewa. Chuki ya kiyahudi juu ya Yesu ilifikia kiasi hicho kwamba, walitamani kuharibu na wafuasi wake nao.

SALA: Bwana Yesu, tunakushukuru kwa sababu wewe ndiwe enzi ya Mungu iliyoingia mwilini. Tulinde saa ya majaribu tusije tukategemea tu usalama na raha zetu kuliko kukutegemea wewe. Tuongoze tufaulu kujikana, na huku tuwe wajasiri na waaminifu; tukubali bora kufa kuliko kukukana au kuacha kukujali.

SWALI:

  1. Kwa nini Wayahudi walikataa uwezekano wa kumponya mtu aliyekuwa haoni tangu kuzaliwa?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:29 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)