Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 056 (Jesus the light of the world)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

d) Yesu, nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12-29)


YOHANA 8:21-22
„Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi zenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja. Basi Wayahudi wakasema, Je, atajiua! Kwa kuwa asema, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja?“

Yesu alifahamu kwamba alizungukwa pande zote na watumishi wa hekalu. Alidokeza kwa maneno ya kuficha maana ya ndani ya mambo yajayo, „Saa ya kufa kwangu imekaribia. Ndipo nitatoka ulimwenguni, na ninyi hamtaweza kunifuata. Ninyi sio wauaji wangu kufuatana na mpango wenu. Mimi naamua saa ya kuondoka kwangu.“

„Lakini nitafufuka toka kaburini nikipita katikati ya miamba na milango iliyofungwa. Mtanitafuta bure, hamtanipata. Nitapaa kwa Baba yangu, wala ninyi hamtaitambua. Mmenikataa, mimi niliye Mwana Kondoo wa Mungu, wala hamkunitegemea, niliye Mwokozi wa wanadamu. Mtaangamia katika kifungo cha dhambi zenu.“ Yesu hakusema, „Mtakufa katika dhambi zenu.“ Dhambi zetu nyingi za kijamii hazithibitishi hatia yetu ya kimsingi, ila zaidi ni jinsi tunavyosimama mbele za Mungu, pia na kutokuamini kwetu ndiyo dhambi yetu.

Wayahudi walitambua kwamba Yesu alisema habari ya kuondoka kwake kabisa, lakini hawakushika ushuhuda wake, kwamba atarudi kwa Baba yake. Bali walidhani kwamba katika mvutano wake na Mafarisayo na makuhani alifikia mwisho wa nguvu zake. Basi asibakie na njia nyingine ila kujiua. Kuzimu au kupotea milele kutammeza kama mtu wa kujiua? Wayahudi walifikiri au kuhisi kwamba hawatashiriki bahati hiyo kwa sababu ya haki zao. Lakini Warumi waliposhinda Yerusalemu mwaka 70 B.C., maelfu ya Wayahudi walijifisha wenyewe kwa ajili ya njaa au kukata tamaa.

YOHANA 8:23-24
„Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu, kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.“

Yesu alitangaza kwamba milki ya Mungu kweli ipo juu ya dunia yetu bovu. Sisi sote tu wa toka chini, kutoka katika udongo, tukijaa mawazo machungu. Mbegu za shetani zinazaa matunda yaliyooza. Mtu wa kawaida hawezi kutambua ufalme wa Mungu, ingawa anabahatika kusikia kwa ndani kwamba kuna kitu cha namna hii.

Kristo sio wa ulimwengu huu. Nafsi yake inatokana na Baba. Alidokeza ufalme wa Babaye mahali pa juu, lakini sio katika utambuzi wa kisayansi ya kijiografia. Kadiri uzito wa vitu unavyopungua, tunavyopaa juu (yaani nguvu ya mvuto wa ardhi inapungua kadiri tunavyoenda juu, kwa mfano ndani ya ndege inapotembea kawaida meta 3000 juu, uzito wa kila kitu kimepungua kiasi fulani), vivyo hivyo jinamizi ya dhambi inapungua hadi kupotea kabisa kadiri tunavyomkaribia Mungu. Dunia yetu ni kama gereza tusioweza kuitoroka. Sisi tu uzazi wa mazingira yetu yanayokataa kujikabidhi kwa upendo wa Mungu. Maisha yetu yamejaa madhambi. Hapo hapo Yesu alitumia neno la dhambi katika namna ya nyingi, yaani ma-dhambi mengi, kwa sababu kutokana na kukataa kwetu kwa Mungu, madhambi mengi na makosa yanajitokeza. Tunafanana na mwenye ukoma, ambaye mwili wake hujaa madonda na makovu. Jinsi maskini huyu anavyokufa polepole, akiwa bado yu hai, ndivyo dhambi inavyomharibu mtu polepole. Tutakufa kwa sababu tumetenda dhambi. Dhambi ni nini? Kwanza ni kutokuamini, maana yule aliyejikabidhi kwake Kristo ataishi milele. Damu ya Mwana wa Mungu inaendelea kumsafisha na dhambi. Nguvu yake inasafisha na dhamiri yetu na kutakasa mawazo yetu. Lakini yeyote aendeleaye kuwa mbali na Kristo anachagua kifo, akidumu ndani ya gereza la dhambi na kungojea hukumu ya milele. Imani ndani ya Kristo peke yake inatuweka huru na ghadhabu ya Mungu.

Yesu basi ni nani atazamiaye imani ndani ya nafsi yake? Hapo napo mwenyewe anajieleza “Mimi ndiye” (Yoh.6:20 na 8:24, hapo juu). Hivyo anajumlisha shuhuda zake zote zilizo kuu juu yake mwenyewe. Alijiita Bwana wa ukweli, Mungu aishiye milele, Aliye Mtakatifu, aliyejifunua kwa Musa ndani ya kichaka kwa maneno hayo hayo: “Mimi niko ambaye niko” (Kutoka 3:14 na Isaya 43:1-12). Wala hakuna wokovu ndani ya mwingine. - Kila Myahudi alifahamu kabisa tamko hizo mbili, bila kuthubutu kuyatamka, asije akatumia jina la Mungu bure. Lakini Yesu alijitaja mwenyewe kwa maneno hayo wazi mbele za watu: Yeye siye Kristo tu, Mwana wa Mungu, bali naye ni Yehova, Mungu wa Kweli.

Yeye ndiye muhtasari wa Injili. Kristo ni Mungu mwilini. Yeyote amwaminiye ataishi milele. Lakini amkataaye na kugoma kukubali uweza wake, anajizuia asipate msamaha. Imani au kutokuamini inaamua kwamba mtu ataishia wapi baada ya kufariki dunia.

SWALI:

  1. Imani ndani ya yule ajiitaye “Mimi ndiye” ina maana gani?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:13 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)