Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 038 (Four witnesses to Christ's deity)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
A - Safari ya pili kwenda Yerusalemu (Yohana 5:1-47) -- Neno Kuu: Kutokea kwa uadui kati ya Yesu na Wayahudi

4. Shuhuda nne juu ya Uungu wa Kristo (Yohana 5:31-40)


YOHANA 5:31-40
31 “Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. 32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. 33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akanishuhudia kweli. 34 Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka. 35 Yeye alikuwa taa iwakayo na kung’aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda. 36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma. 37 Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkusikia wakati wo wote, 38 wala sura yake hamkuiona. Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye. 39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. 40 Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.”

Yesu aliwatangazia adui zake kwamba, anayo mamlaka kutenda kazi za Masihi aliyeahidiwa. Wao walimchukia huyu mtu wa shambani aliyevuruga taratibu zao na kanuni zao. Basi waliulizia ushuhuda wa kuthibitisha madai yake. Yesu alijinynyekeza kuitikia ulizo lao kwa mathibitisho. Sisi sote twajifikiria kuwa bora kuliko tulivyo kwa hali halisi. Ila Yesu alitoa maelezo kweli kabisa juu yake mwenyewe bila alama yoyote ya udanganyifu. Ushuhuda wake ni wa kweli, ingawa kisheria ni kawaida kutokuhesabu ushuhuda wa mtu juu yake mwenyewe. Hali hii Yesu alithibitisha mwenyewe kwa kusema, “Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.” Yeye hakuhitaji kujikinga mwenyewe, kwa vili mwingine alikuwa amemshuhudia, ambaye ni Baba yake wa mbinguni; na yeye akamsimamia na alama ya mara nne, au mistari minne ya ushuhuda.

Mungu alimtuma Mbatizaji ili amtangaze Kristo kati ya watu. Huyu mtangulizi alimshuhudia Kristo na huduma yake kama kuhani na huduma yake kama Mhukumu. Hata hivyo, baraza hilo la juu lilimtia mashaka Yohana na kukataa ushuhuda wake kumhusu Yesu (Yoh.1.19-28). Shuhuda za Yohana Mbatizaji hazikuwa madhumuni ya Yesu, wala si mwongozo wa nia yake, bali Yesu alikuwa yule aliyekuwa tangu milele. Kwa sababu ya kutokuelewa kwa watu, Yesu alikubali ushuhuda wa Mbatizaji kama nyongeza juu ya ukweli wake. Mbatizaji “hakutia chumvi” alipomweleza Yesu kuwa ni Mwana Kondoo wa Mungu na mtoaji wa Roho.

Mbatizaji alikuwa ni taa iliyong’aa usiku, akikusanya kundi la wafuasi karibu naye wapate kumulikiwa. Lakini jua lilipochomoza kwa njia ya nafsi ya Yesu, hapakuwana haja tena ya taa. Yesu pekee ndiye nuru ya ulimwengu, akiwa na nguvu ya kung’aa bila kukoma. Kama vile jua linavyoleta uhai na kukua kwa mimea yote, ndivyo Yesu anavyoleta uhai wa kiroho na upendo. Kuponya wagonjwa kwake na kuishi kwake kulionyesha ushindi wake wa nuru na kushinda giza. Kutuliza kwa dhoruba ziwani na kufufua kwa wafu kulithibitisha Uungu wake. Kazi zake zilikuwa katika moyo mmoja na Baba. Alikamilisha huduma yake msalabani, na kwa kufufuka kwake alimiminia Roho Mtakatifu juu ya wale walioomba. Matendo ya Mungu yatakamilika katika kuja kwake Kristo mara ya pili, yaani kuwafufua wafu na kuhukumu ulimwengu. Hakuna tofauti kabisa kati ya Baba na Mwana katika kutenda kazi kwao: Jinsi Baba anavyotenda hadi leo, ndivyo na Mwana anavyotenda pia.

Mungu mwenyewe alipaza sauti yake kwa ajili yetu ili tusikie thibitisho lake kuu: “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye.” (Math.3:17). Hakuna aliyepokea ushuhuda kama huu ila Yesu tu, ambaye tangu milile aliishi kufuatana na mapenzi ya Mungu. Mwana mpendwa alikuwa amejaa upendo wa kweli na usafi.

Yesu aliwaambia Wayahudi kwamba hawajamjua Mungu. Walishindwa kutambua sauti yake ndani ya torati na manabii. Hawakuona sura yake wazi ndani ya maono au ndoto. Mafunuo yote yaliyotangulia hayakuwafaa, kwa vile dhambi zao ziliwatenganisha naye aliye Mtakatifu. Jinsi Isaya alivyolia alipoona tu upinde wa vazi la Mungu hekalini: “Ole wangu! Kwa maana nimepotea, kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu..” Thibitisho la uziwi wao wa kiroho na upungufu wa ufahamu ilikuwa ni kumkataa Kristo, aliyekuwa ni Neno la Mungu mwilini. - Yeyote anayejidhania kwamba anafahamu Neno la Mungu, na huku anamkataa Yesu aliye Neno la Mungu, basi anahakikisha kwa hilo kwamba hajapokea ufunuo halisi, au hajaufahamu kabisa.

Watu wa Agano la Kale walichunguza maandiko, wakitazamia kuona njia ya uzima wa milele mle. Badala yake walikuta maneno ya sheria yasiyo na uhai. Na walikosa kuona zile ahadi zilizoelekeza kwa Masihi, ingawa matabiri ya namna hii yako mengi ndani ya Agano la Kale. Walipendelea mawazo yao wenyewe, mafafanuzi na kanuni zao, huku wakishindwa kutambua kwamba, Kristo ndiye Neno la mwisho la Mungu, tena tayari alikuwa amefikia katikati yao.

Yesu aliwaonyesha sababu ya kukataa kwao - ni kutokumtaka Mungu jinsi alivyo kweli. Walimchukia Kristo na hivyo kukosa uzima wa milele, na kukosa shabaha ya imani na neema.

SALA: Bwana Yesu, twakushukuru kwa kuwa unawapenda hata adui zako; ulihuzunika kwa sababu ya kutokuamini kwao. Uliwaonyesha ushuhuda za namna nne kuhusu Uungu wako. Tusaidie kuchunguza injili na maandiko mengine ya Biblia, ili tukuone na kuvumbua Uungu wako, na tutegemee kweli matendo yako na kupokea uzima wa milele. Twaomba ufungue masikio ya mamillioni ya watu ambao bado ni viziwi kwa kusikia sauti yako siku hizi.

SWALI:

  1. Zipi ni zile shuhuda nne, na kwa jambo gani zinashuhudia?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 31, 2013, at 10:12 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)