Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 032 (Healing of the court official's son)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
C - Kristo kutembelea mara ya kwanza mji wa Yerusalemu (Yohana 2:13 - 4:54) -- Neno Kuu: Kuabudu kwa kweli ni nini?

5. Kumponya mwana wa diwani (Yohana 4:43-54)


YOHANA 4:43-46a
43 “Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya. 44 Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe. 45 Basi alipofika Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yeruaslemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu. 46a Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai.”

Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamehubiri kule Samaria. Kwa nguvu ya uhai wa milele na furaha walifanya kazi ya uinjilisti. Wakati wa kuwafikia watu wa mataifa ilikuwa ni bado; ilimpasa kwanza kupambana na roho mbaya kwenye nchi yake ya nyumbani. Akaenda moja kwa moja Galilaya, ingawa wenyeji wa Nazareti walimdhihaki pamoja na uwezekano wa kugongana nao. Watu wa ukoo wake na marafiki bado hawakuamini utukufu wake, maana alizaliwa katika familia ya chini. Wao walitamani utajiri na fahari na kudharau umaskini wa Yesu. Hakuweza kufanya mwujiza kati yao kwa sababu walimhisia hivyo.

Ila sifa zake kama mponyaji ilienea haraka na mpaka mbali. Habari ya miujiza yake alizozitenda Yerusalemu na Galilaya ilimtangulia. Wagalilaya wengi walikuwa wametembelea Yerusalemu siku za Pasaka. Walisikia na kuona yote aliyoyatenda na kusema, jinsi alivyohubiri na madaraka makuu. Walimfurahia alipofikia tena vijiji vya Galilaya, wakitamani atende na miujiza mingine kati yao, ili wapate kufaidika naye. Yesu akarudia tena nyumbani kwa yule bwana arusi kule Kana, ambapo furaha ya arusi ile ikawa neno kuu la kuvutia. Alipenda kukamilisha huduma yake kwa wale walioanza kumtazama kwa tegemeo njema kutokana na mwujiza wake wa kwanza kule Kana.

YOHANA 4:46b-54
46b “Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. 47 Huyo aliposikia ya kwamba Yesu alikuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; maana alikuwa kufani. 48 Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? 49 Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. 50 Yesu akamwambia: Enenda, mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia. 51 Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. 52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, jana saa saba homa ilimwacha. 53 Basi Babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile lie aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini na wote wa nyumbani mwake. 54 Hivyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.”

Mtu wa maana wa baraza la Mfalme alimfikia Yesu, akiwa amesikia habari zake na mamlaka yake. Wenyeji wa kijiji kile wakasikia habari ya kufika kwake na kusema: “Anamwelekea mponyaji ili amjulishe kwa Mfalme.”

Huyu diwani alikuwa na mwana hawezi kule Kapernaumu, ufuoni mwa ziwa Galilaya. Baba alikuwa amewajaribu madaktari kadhaa, akitumia hela nyingi, lakini mtoto wake bado hajapona. Kwa nafasi ya mwisho alimjaribu Yesu; je ataweza kumsaidia au hapana? Yule Baba alimtaka Yesu atoke Kana na kwenda naye Kapernaumu, akitegemea kwa kuwepo kwake mwana wake atapata kupona.

Yesu hakushughulika kumsalimia huyu ofisa mkuu. Alisikitika tu kwamba huyu naye alionyesha upungufu wa imani. Yesu anashindwa kusaidia, hadi mtu aamini kwa kweli habari za mamlaka yake isiyo na mfano. - Wengi huomba na kuamini, lakini wakati uo huo wanatamani kupatiwa msaada wa kimwili tu. Mwumini wa kweli wa Bwana hutegemea kabisa neno lake bila masharti, akiamini hata kabla ya msaada kufika.

Diwani hakuudhiwa kwa kukemewa na Yesu, bali alinyenyekea kwake kwa kusema: “Bwana”, au “Mkuu”, ambalo kwa desturi za Kiyunani alijifanya mwenyewe kuwa mtumishi kwake Kristo. Upendo wake kwa mwanawe pamoja na heshima kwa Yesu zilimwongoza tena amwulize Yesu, tafadhali njoo Kapernaumu, ili uokoe uhai wake.

Kwa hali hii Yesu alitambua haja kuu ndani ya huyu diwani ya kumwamini pia na ukuu wake, akamwambia: “Nenda, mwana wako ataishi”. Yesu alikataa kwenda na huyu diwani hadi Kapernaumu, lakini alipima upendo wa yule baba na kuimarisha imani yake; je, atakuwa na tumaini ndani ya uwezo wa Yesu kuponya, iwapo kulikuwa na umbali kati yao na mtoto mgonjwa?

Wakati wa maongezi haya diwani alitambua enzi ya Yesu na upendo wake. Alijihakikishia kwamba Yesu hasemi uongo wala hakumchokoza tu. Basi akaamini ingawa hakuweza kushuhudia kwa macho kupona kwa mwanawe. Kwa kumtii Yesu akaanza safari ya kurudi Kapernaumu. Kuondoka kwake kwa utii kulimheshimu Yesu na kuthibitisha uponyaji ule. - Iwapo Yesu aliweza kuponya hivyo mwana aliyekuwa karibu na kufa, basi yeye ni mkubwa kuliko wote wengine. Kule kuponya kulithibitisha mamlaka yake na asili yake tukufu. Hivyo safari yake ya kurudi kipekee ilikuwa mazoezi ya kukuza tumaini lake.

Yesu naye aliwasukuma watumishi wa diwani wakimbie kwake na kumtangazia kwamba mwanawe amepona kabisa. Hofu zake zilipotea haraka akamtukuza Bwana. Akiwa na hamu ya kuhakikisha habari ya saa ambapo homa ilimwacha mwanawe, akaambiwa ilikuwa ni mchana saa saba, wakati ule ule Yesu alipotamka kupona kwake na ahadi yake.

Basi huyu diwani alishuhudia nyumbani kwake mambo yote pamoja na moyo wa shukrani habari ya nguvu ya upendo wa Kristo.

Tukio hilo la kimwujiza ilikuwa ni tendo la pili la ajabu, ambalo Mwinjilisti Yohana anatusimulia. Mvuto huo wa Kristo sasa ilienea maofisini kwa Mfalme. Kwa hamu watu waliangalia mbele kwa mengine yatakayotendeka. Walianza kumwamini Kristo na kutegemea njia hii itakubalika na Mungu, aliyethibitisha hayo kwa njia ya miujiza na matendo ya nguvu.

SALA: Bwana Yesu, twakushukuru sana kwa kuja kwako. Ulimwokoa kijana yule aliyekuwa karibu kufa kule Kapernaumu, ingawa hukuwepo pale wewe mwenyewe. Ulimwongoza baba yake apate imani imara ndani yako. Tufundishe kutegemea kabisa upendo na enzi yako.Tunaombea waokolewe wengi waliokufa dhambini na wenye upotovu. Tunaamini kwamba unajibu maombi yetu.

SWALI:

  1. Zipi ni hatua za kukua kiimani, ambazo yule diwani alizipitia?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 31, 2013, at 09:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)