Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 013 (The Sanhedrin questions the Baptist)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

1. Utume kutoka kwa baraza kuu (iitwayo Sanhedrin) unamhoji Mbatizaji (Yohana 1:19-28)


YOHANA 1: 25-28
25 „Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi unabatiza, ikiwa wewe si Kristo. wala Elija, wala nabii yule? 26 Yohana akawajibu, akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Kati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. 28 Hayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya Jordani alikokuwako Yohana akibatiza.“

Wayahudi walijifunza kutokana na torati habari ya utakaso, kuoshwa na aina ya ubatizo. Ubatizo ambao wamezoea ulikuwa kuoshwa na mambo kadhaa machafu. Lakini kwao ubatizo wa kweli ulikuwa kwa watu ambao si Wayahudi, wakitaka kuungana na dini yao, kwa sababu waliwahesabu watu wote wa mataifa kuwa chafu ki-dini. Hata hivyo, kubatizwa kulikuwa ni alama ya kunyenyekea na kuungana na taifa la Mungu.

Hii inaonyesha vile wajumbe toka Yerusalemu walivyoshangaa na kuuliza: “Kwa nini unawaita waumini kutubu, watu ambao wametahiriwa na kukamilika ndani ya Agano? Unatuchukulia kwamba sisi hatutoshi katika utakatifu na kufikiri kwamba, tumepotea chini ya hasira ya Mungu? Sisi tulio na wajibu mkubwa kama viongozi katika taifa letu?

Ubatizaji wa Yohana ulikuwa kikwazo kikubwa kwa watu waliojidhania kuwa wasafi. Basi, waligawanyika katika vikundi viwili. Kikundi cha kwanza ni wale waliotakasika kupitia ubatizo wa kutubu dhambi. Hao walikuwa wamejitenga kando, ili kujitayarisha wamlaki Bwana wao. Kikundi cha pili walikataa ubatizo wa toba, wakijisikia kuwa tayari kumpokea Kristo akija. Walidhania kwamba, kuja kwake kulikuwa kwa shabaha za kisiasa au za kisheria.

Pengine Mwijilisti Yohana mwenyewe alikuwapo pale walipoamua hivyo na kugawanyika. Kuhojiana kwao kulimkera sana, hasa maswali ya wajumbe kwa Mbatizaji. Maana kwa maswali yao walidhihirisha kwamba, yeye si Kristo wala Eliya wala Nabii yule wa ahadi. Kupitia majibu yao walimwudhi wakisema yeye si kitu.

Mbatizaji yule, akijua la kufanya, alijinyenyekeza na kusema, “Ninyi ni wenye haki, mimi sina umuhimu. Ninabatiza na maji tu bila uchawi au uwezo fulani. Yote ninayofanya ni dhihirisho tu, nikieleza kwa yule anayekuja.” Ndipo Mbatizaji katika nguo za nywele za ngamia alisimama na kutangaza kwa sauti kubwa kwa viongozi wa ujumbe ule na kwa kusanyiko lote. “Ninyi nyote ni vipofu! Mmeshindwa kutambua mambo ya historia, ambayo yanafanyika kati yenu. Mnanihoji mimi ambaye si kitu, wala sina uwezo. Tazameni, Kristo amekwisha kufika! Yuko hapa katikati ya mati ya wanaotubu. Mimi niko nikifanya huduma moja tu. Mimi ni sauti tu, na Roho Mtatatifu amenijulisha juu ya yule Bwana anayekuja sasa. Hapa hapa yupo! Na leo ni siku ya wokovu. Ungameni haraka, kwa sababu dakika za mwisho zimewadia!”

Kwa kutoa taarifa hii makusanyiko walipagawa kwa hofu. Walikusanyika wakiwa na shabaha ya kumkaribisha Kristo Lakini tayari, alikuwa amekwisha kufika! Nao hawakutambua kuingia kwake wala kumwona. Walikuwa wa kuchanganyikiwa, wakiangaliana wao kwa wao kwa mshangao.

Hapo Mbatizaji alitamka habari ya Kristo kwa ushuhuda wa undani kuliko vile mwandishi wa injili alivyomtaja Kristo katika aya ya kumi na tano: “Yule anayekuja baada yangu alikuwapo kabla yangu”. Hivyo Mbatizaji alidhihirisha umilele wa Kristo, na pia kuwapo kwake hapo hapo kati yao. Aliweka wazi kwamba, kwa sura ya nje Kristo ni mtu wa kawaida, na anakaa kati yao bila kutambulikana, bila duara ya mwangaza kichwani, wala kuelezwa kwa mavazi yake, ama macho ya moto. Yeye hakuwa tofauti na wengine, wala kutofautiana kwa namna yoyote. Lakini kwa utu wake wa kweli alikuwa tofauti kabisa na mtu yeyote. Mwenye uhai kabla ya enzi zote, mwenye hali ya kimbinguni na tukufu, na hata hivyo amesimama katikati yao kama mtu wa kawaida.

Mbatizaji alikiri kwamba hastahili kuwa mtumishi wake Kristo. Kulingana na utamaduni wa wakati ule ni kwamba, wageni wakingia nyumbani, mtumishi aliwaosha miguu kwa maji. Kumwona Yesu amekuja kwa mkutano, Yohana hakujiona angefaa kufungua gidamu ya viatu vyake Kristo, ili aoshe miguu yake.

Maneno haya yaliwashangaza watu sana. Wakaulizana wao kwa wao, “Ni nani huyu mgeni aliye karibu nasi? Bwana anawezaje kuwa mtu wa kawaida? Na kwa nini Mbatizaji anasema hastahili hata kufungua gidamu ya viatu vyake?” Wajumbe toka Jerusalemu labda walidharau maongeo ya Mbatizaji na kama kusema: “Huyu Mbatizaji mnyonge bila shaka ni mdanganyi.” Wakaenda zao. Hata baadhi ya wafuasi wake wakafuatana nao, wakifikiri Kristo atatokea katika jiji lao la Yerusalem kwa hali ya mwangaza na enzi, wala si kama mtu ambaye hajulikani, wa kawaida na anayetokea jangwani. Hivyo walikosa nafasi nzuri ya kukutana na Kristo, mwana wa Mungu.

Mambo haya yalifanyika mashariki ya ukingo wa mto Yordani, nje ya mamlaka ya baraza la wazee wa Sanhedrin, sehemu iliyokuwa chini ya utawala wa Herode Antipa. Hivyo Wajumbe hawakuweza kumkamata Mbatizaji na kumleta ahukumiwe pale Jerusalem.

SALA: Bwana Kristo Yesu, ninakushukuru kwa kuja kwako kwetu, uliye mwanadamu kamili na Mungu wa milele. Tunakuabudu na kuliinua jina lako kwa kutuleta karibu nawe. Ulinyenyekea kimwili kiasi kwamba hakuna mtu aliyekutambua ila Mbatizaji tu. Wewe ndiwe mnyenyekevu na mpole kimoyo. Tufunze nasi kunyenyekea kama wewe na kukufuata kufuatana na uongozi wa Roho Mtakatifu.

SWALI:

  1. Nini ilikuwa kilele cha ushuhuda wa Mbatizaji kwa Yesu mbele ya wajumbe wa baraza la wazee wa wayahudi, iitwayo “Sanhedrin”

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)